download from google play download from apple store
Connection failed Try again
download from google play download from apple store

Mbatia: Sijatumwa na Magufuli kuiangusha Chadema Mbeya

mwananchi.co.tz 03/7/2020

Mbeya. Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia amesema mazungumzo yake na Rais wa Tanzania, John Magufuli ya Machi 3, 2020 Ikulu jijini Dar es Salaam hayakulenga kukiangusha Chadema katika majimbo ya Rungwe, Busokelo na Kyela katika uchaguzi mkuu wa Oktoba, mwaka huu.

"Nimekuja Mbeya kwenye ziara ya kukiimarisha chama cha NCCR si kwamba nimetumwa na Rais John Magufuli kuja kukiua Chadema. Hiyo ni hofu yao, majungu na ufike wakati kujenga hoja za fikra,” amesema Mbatia leo Jumamosi Machi 7, 2020 katika mkutano na waandishi wa habari mjini Mbeya.

Amebainisha kuwa ziara yake mkoani humo ni kwa ajili ya kukiimarisha chama na kuangalia changamoto zinazowakabili wananchi katika majimbo hayo.

Machi 3, 2020 katika kinachoweza kutafsiriwa kuwa ni kuibua matumaini mapya ya maridhiano, Rais Magufuli alikutana na kufanya mazungumzo na viongozi watatu wa vyama vya upinzani Ikulu, Dar es Salaam.

Mazungumzo hayo yalijikita katika masuala ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 na kuhimiza haja ya kudumisha amani, usalama na upendo.

Viongozi waliokutana na Rais kwa nyakati tofauti ni mshauri mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo,  Maalim Seif Sharif Hamad;  Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba na Mbatia.

Hata hivyo, haikueleweka mara moja kama kukutana huko kutakuwa na mwendelezo wa vikao vingine vya viongozi wengine wa upinzani.

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa alipoulizwa kwa simu alisema suala hilo ni siri ya ratiba za rais.

Baada ya asubuhi viongozi hao kukutana na Rais, mchana Mbatia alikutana na waandishi wa habari na kumpokea katibu mwenezi wa zamani wa Baraza la Vijana Chadema (Bavicha), Edward Simbeye  na kisha kutangaza kuanza ziara ya kukiimarisha chama hicho.

Katika mkutano wa leo, Mbatia amesema, “nimefanya ziara katika jimbo la Rungwe, Busokelo na Kyela kimsingi nimejionea hali halisi barabara mbovu, uchafu na kwetu sisi kama NCCR tunataka kusimamisha wagombea katika nafasi zote za udiwani, ubunge na urais ili kujenga utu, ujamaa na umoja wa Watanzania.”

Mbatia amesema vyama vya siasa  nchini vinajidanganya kama ni bora kuliko vyama vingine na kwamba hakuna chama wala serikali yenye nchi, “bali kila chama kina haki ya kushika dola  na kuongoza wananchi na ndio maana mwalimu Nyerere (Julius) aliingiza mfumo wa vyama vingi ambavyo vinapaswa kushindana na hoja na si matusi, kejeli na propaganda zisizo na maslahi mapana kwa Watanzania.”

Habari mpya

GSM:TUNATAKA KUACHA ALAMA YANGA, SEVILLA WATATUNGAZIA NCHI, MKATABA WASAINIWA

42min salehjembe.blogspot.com

GSM:TUNATAKA KUACHA ALAMA YANGA, SEVILLA WATATUNGAZIA NCHI, MKATABA WASAINIWA

Siri Ushindi wa Magufuli dhidi ya Corona Yafichuka - Global Publishers

2d globalpublishers.co.tz

Siri Ushindi wa Magufuli dhidi ya Corona Yafichuka - Global Publishers

Jinsi ya kumfanya mpenzi wako ajisikie na penzi lako

bongoleo.com

Jinsi ya kumfanya mpenzi wako ajisikie na penzi lako

Serikali yatoa mwongozo wa kudhibiti corona Vyuoni, Shule za Msingi na Sekondari

2d bongo5.com

Serikali yatoa mwongozo wa kudhibiti corona Vyuoni, Shule za Msingi na Sekondari

Polisi Yaaingilia Sakata la Mwanamke Anayeidaiwa Kufumaniwa na Mume wa Mtu - Global Publishers

5d globalpublishers.co.tz

Polisi Yaaingilia Sakata la Mwanamke Anayeidaiwa Kufumaniwa na Mume wa Mtu - Global Publishers

Huyu ndio mwanamke wa kuoa, ila sijui kama Tanzania yupo

edusportstz.com

Huyu ndio mwanamke wa kuoa, ila sijui kama Tanzania yupo

VIDEO: BINTI ALIYEBAKWA na MCHUNGAJI hadi MIMBA, Asimulia

2d globalpublishers.co.tz

VIDEO: BINTI ALIYEBAKWA na MCHUNGAJI hadi MIMBA, Asimulia

Virusi vya corona: Rais wa Tanzania anasema wagonjwa wanapungua, je yuko sahihi?

bbc.com

Virusi vya corona: Rais wa Tanzania anasema wagonjwa wanapungua, je yuko sahihi?

Msichana aliyerekodi video ya yule Polisi akimuua Mmarekani mweusi, Adaiwa kupata kiwewe

2d bongo5.com

Msichana aliyerekodi video ya yule Polisi akimuua Mmarekani mweusi, Adaiwa kupata kiwewe

FAIDA ZA KUNYWA MAJI ASUBUHI KABLA YA KULA CHOCHOTE

lemutuz.co.tz

FAIDA ZA KUNYWA MAJI ASUBUHI KABLA YA KULA CHOCHOTE
Related news

Kauli ya CHADEMA kuhusu mgombea Urais

5d muungwana.co.tz

Kauli ya CHADEMA kuhusu mgombea Urais

Magufuli apiga marufuku uvaliaji wa barakoa nchini Tanzania

6d radiojambo.co.ke

Magufuli apiga marufuku uvaliaji wa barakoa nchini Tanzania

Siri Ushindi wa Magufuli dhidi ya Corona Yafichuka - Global Publishers

2d globalpublishers.co.tz

Siri Ushindi wa Magufuli dhidi ya Corona Yafichuka - Global Publishers

TAHARIRI: Ukaidi wa Tanzania tishio kwa eneo zima

taifaleo.nation.co.ke

TAHARIRI: Ukaidi wa Tanzania tishio kwa eneo zima

Rais Magufuli atangaza kufunguliwa kwa vyuo vikuu na shule za sekondari Tanzania

8h kiswahili.tuko.co.ke

Rais Magufuli atangaza kufunguliwa kwa vyuo vikuu na shule za sekondari Tanzania

Picha : RAIS MAGUFULI AWAKABIDHI ZAWADI YA TAUSI MARAIS WASTAAFU WA TANZANIA

1d malunde.com

Picha : RAIS MAGUFULI AWAKABIDHI ZAWADI YA TAUSI MARAIS WASTAAFU WA TANZANIA

Atangaza kugombea urais kupitia Chadema

4d habarileo.co.tz

Atangaza kugombea urais kupitia Chadema

Lissu awacharua wabunge waliotimka Chadema na kuanza kutoa tuhuma kwa Mbowe

bongoleo.com

Lissu awacharua wabunge waliotimka Chadema na kuanza kutoa tuhuma kwa Mbowe

Dunia imeanza kumwelewa Rais Magufuli

rai.co.tz

Dunia imeanza kumwelewa Rais Magufuli

Ngoma nzito wabunge 15 Chadema

mtanzania.co.tz

Ngoma nzito wabunge 15 Chadema