download from google play download from apple store
Connection failed Try again
download from google play download from apple store

Polisi yasema aliyeuawa Singida hakuwa kiongozi wa Chadema

mwananchi.co.tz 02/27/2020

Singida. Jeshi la Polisi mkoani Singida limesema dereva wa bodaboda, Alex Jonas (40) aliyeuawa na watu wasiofahamika alikuwa siyo kiongozi wa Chadema.

Jonas ambaye ni mkazi wa Majengo mjini Manyoni mkoani  Singida mwili wake ulikutwa umepigwa na kitu chenye ncha kali Februari 25, 2020.

Akizungumza na Mwananchi leo Alhamisi Februari 27, 2020 ofisini kwake Kamanda wa Polisi, Sweetbert Njewike amesema dereva huyo ameuawa Februari 25 mwaka huu nyakati za usiku.

Amesema kijana huyo ambaye kituo chake cha kazi kilikuwa Mwembeni mjini Manyoni bado haijafahamika siku ya tukio, aliondoka muda gani.

Kamanda Njewike amesema mwili wa marehemu uliokotwa mbungani mbali na barabara, ukiwa umechomwa chomwa sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo kichwani na miguuni.

“Wakati mwili wa Alex ukiokotwa mbungani, pikipiki yake iliokotwa kandakando ya barabara iendayo Dodoma. Baada ya mwili kukaguliwa alikutwa na vitu vyote isipokuwa simu. Chanzo cha mauaji hayo bado hakijafahamika, upelelezi unaendelea,” amesema.

Amesema hadi sasa hakuna mtu anayeshikiliwa kuhusiana na mauaji hayo ya kikatili na wameanzisha msako mkali.

“Tunaomba mwananchi yeyote mwenye taarifa sahihi juu ya tukio hilo atoe kwenye kituo chochote cha polisi kilicho karibu au mamlaka zingine ili watu\mtu aliyehusika aweze kukamatwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria,” amesema.

Kuhusu marehemu kuwa kiongozi wa Chadema wilayani Manyoni, Njewike amesema hilo wamelisikia lakini walipofanya utafiti imebainika kuwa alikuwa ni dereva wa bodaboda tu na sio kiongozi wa Chadema.

Wakati Kamanda Njewike akisema kuwa Alex hakuwa kiongozi wa Chadema, Mwenyekiti CCM Halmashauri ya Itigi, Alli Minja akizungumza na Mwananchi amesema marehemu Alex alikuwa mwenyekiti Chadema Wilaya ya Manyoni.

“Binafsi nasikitika kwamba sitohudhuria mazishi yake kutokana na kukosa usafiri. Alex alikuwa Chadema wa aina yake,” amesema na kuongeza;

“Alikuwa na utamaduni wa kuhudhuria vikao vya mabaraza ya madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni na kwetu huku Itigi. Kwenye suala la miradi ya maendeleo, ulikuwa huwezi kujua kama ni wa upinzani. Alikuwa anatoa ushirikiano wa hali ya juu. Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi,” amesema Minja.

Akizungumza leo na Mwananchi, mmoja wa viongozi wa Chadema Kanda ya Kati, Idd Kizota amesema wapo katika maandalizi ya mazishi ambayo yatafanyika wilayani humo Jumamosi, Machi 1, 2020.

Habari mpya

Faida saba(7) zitokanazo na juisi ya ukwaju

4d muungwana.co.tz

Faida saba(7) zitokanazo na juisi ya ukwaju

Jinsi ya kumfanya mpenzi wako ajisikie na penzi lako

bongoleo.com

Jinsi ya kumfanya mpenzi wako ajisikie na penzi lako

Siri Ushindi wa Magufuli dhidi ya Corona Yafichuka - Global Publishers

2d globalpublishers.co.tz

Siri Ushindi wa Magufuli dhidi ya Corona Yafichuka - Global Publishers

Serikali yatoa mwongozo wa kudhibiti corona Vyuoni, Shule za Msingi na Sekondari

2d bongo5.com

Serikali yatoa mwongozo wa kudhibiti corona Vyuoni, Shule za Msingi na Sekondari

Njia ya kutunza mayai kwa njia ya asili

1h muungwana.co.tz

Njia ya kutunza mayai kwa njia ya asili

Virusi vya corona: Rais wa Tanzania anasema wagonjwa wanapungua, je yuko sahihi?

bbc.com

Virusi vya corona: Rais wa Tanzania anasema wagonjwa wanapungua, je yuko sahihi?

Msichana aliyerekodi video ya yule Polisi akimuua Mmarekani mweusi, Adaiwa kupata kiwewe

2d bongo5.com

Msichana aliyerekodi video ya yule Polisi akimuua Mmarekani mweusi, Adaiwa kupata kiwewe

FAIDA ZA KUNYWA MAJI ASUBUHI KABLA YA KULA CHOCHOTE

lemutuz.co.tz

FAIDA ZA KUNYWA MAJI ASUBUHI KABLA YA KULA CHOCHOTE

GSM:TUNATAKA KUACHA ALAMA YANGA, SEVILLA WATATUNGAZIA NCHI, MKATABA WASAINIWA

2h salehjembe.blogspot.com

GSM:TUNATAKA KUACHA ALAMA YANGA, SEVILLA WATATUNGAZIA NCHI, MKATABA WASAINIWA

SAA 7 MCHANA...Hawa nyota sita mali ya Simba

mwanaspoti.co.tz

SAA 7 MCHANA...Hawa nyota sita mali ya Simba
Related news

Kauli ya CHADEMA kuhusu mgombea Urais

5d muungwana.co.tz

Kauli ya CHADEMA kuhusu mgombea Urais

Siri Ushindi wa Magufuli dhidi ya Corona Yafichuka - Global Publishers

2d globalpublishers.co.tz

Siri Ushindi wa Magufuli dhidi ya Corona Yafichuka - Global Publishers

Msichana aliyerekodi video ya yule Polisi akimuua Mmarekani mweusi, Adaiwa kupata kiwewe

2d bongo5.com

Msichana aliyerekodi video ya yule Polisi akimuua Mmarekani mweusi, Adaiwa kupata kiwewe

Atangaza kugombea urais kupitia Chadema

4d habarileo.co.tz

Atangaza kugombea urais kupitia Chadema

Ukatili wa polisi wa Marekani dhidi ya Wamarekani weusi, wasababisha kifo cha mtu mwingine

4d muungwana.co.tz

Ukatili wa polisi wa Marekani dhidi ya Wamarekani weusi, wasababisha kifo cha mtu mwingine

Ngoma nzito wabunge 15 Chadema

mtanzania.co.tz

Ngoma nzito wabunge 15 Chadema

ALIYEMPIGA MWANAMKE MWENZAKE KISA KUMFUMANIA ASAKWA NA POLISI

4d lemutuz.co.tz

ALIYEMPIGA MWANAMKE MWENZAKE KISA KUMFUMANIA ASAKWA NA POLISI

Mbaya wa Simba apewa mkono wa kwaheri

mwanaspoti.co.tz

Mbaya wa Simba apewa mkono wa kwaheri

Vitunguu saumu, limao na tangawizi zinavyosaidia kukabili corona

habarileo.co.tz

Vitunguu saumu, limao na tangawizi zinavyosaidia kukabili corona

Mwanahabari wa CNN akamatwa akiripoti moja kwa moja kuhusu maandamano

1d kiswahili.tuko.co.ke

Mwanahabari wa CNN akamatwa akiripoti moja kwa moja kuhusu maandamano